Msafara wa kiongozi wa Azimio la umoja “one Kenya” Raila Odinga umeshambuliwa kwa kupigwa na mabomu ya machozi katika eneo la Kawangare walipokua wakiendelea na maandamano kama alivyoahidi wiki iliyopita kuwa wataandamana kila Jumatatu na Alhamisi.
Dakika chache baada ya maandamano hayo kupita katika eneo la Kawangare maafisa wa polisi waliwarushia vitoa machozi waandamanaji waliokuwa katika msafara huo.
Katika msafara huo Raila Odinga aliambatana na viongozi wengine mbalimbali akiwepo makamu wake Martha Karua, kiongozi wa “Roots party” George Wajackoyah na viongozi wengine.
Ikumbukwe kuwa maandamano hayo yalianza wiki iliyopita ya kupinga hali ya juu ya maisha iliyopo sasa nchini Kenya.