Kiongozi wa upinzani nchini Kenya kutoka chama cha Azimio la Umoja One amesema uvamizi uliofanywa kwenye shamba la Raisi mstaafu Uhuru Kenyatta umefanywa na serikali ya Raisi William Ruto.
Kiongozi huyo amelaani uvamizi huo uliofanywa na makundi ya Wahalifu walioiba na kuchinja baadhi ya mifugo ikiwemo Mbuzi na Kondoo waliokuwa ndani ya Shamba hilo.
Akizungumza na BBC, Odinga amesema uvamizi huo uliofanywa Machi 27, 2023 ikiwa ni siku ya pili ya Maandamano yanayoongozwa na Upinzani haukuwa mpango wao kwenye harakati za kutetea Katiba na kutaka Gharama za Maisha zishuke.
Aidha, amesema yuko tayari kuzungumza na Rais Willima Ruto kwa masharti mawili, ambayo ni Kuruhusiwa kukagua Seva za Tume ya Uchaguzi (IEBC), na kuhakikisha Uteuzi wa Makamishna wapya wa Tume hiyo unapaswa kuhusisha vyama vyote.