ZINAZOVUMA:

Neymar atimkia Al Hilal ya Saudi Arabia

Nyota wa Brazil na PSG Neymar amefikia makubaliano na klabu...

Share na:

Nyota wa Brazil na klabu ya Paris Saint Germain PSG Neymar amekubaliana na klabu ya Al Hilal ya nchini Saudi Arabia kuingia mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.

Staa huyo kwa sasa anamalizia kufanya vipimo vya mwisho vya afya ili aweze kujiunga na timu yake mpya.

Taarifa kutoka PSG zinasema , Neymar alitakiwa kuuzwa toka madirisha matatu yaliyopita ya usajili kwa kile kinachoonekana kuwa sio mchezaji wa kutegemewa tena ndani ya klabu hiyo.

PSG walimsajili nyota huyo kutoka Barcelona kwa £ 200 milioni mwaka 2017 lakini usajili huo wa gharama hakufikia matatajio yao kutokana na kiwango cha mchezaji huyo kuwa cha kawaida.

Aidha klabu mbalimbali kutoka nchini Saudi Arabia zimekua kivutio kwa kuwachukua wachezaji kutoka Bara la Ulaya, mpaka hivi sasa zaidi ya wachezaji 50 kutoka klabu mbalimbali Ulaya wamejiunga na vilabu vya Saudi Arabia.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,