ZINAZOVUMA:

Nchi za Afrika zapanga kuongeza uwekezaji rasilimali watu

Tanzania ni mwenyeji wa mkutano unaoratibiwa na Benki ya Dunia...

Share na:

Wakuu wa nchi na serikali kutoka nchi 21 za Afrika wamethibitisha kushiriki katika mkutano maalumu wa kujadili rasilimali watu utakaofanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akizungumza na chombo cha habari cha uingereza BBC.

Safari ya mkutano huo ilianza tangu Mei 19,2023 na unatarajiwa kufungwa tarehe 26 Julai, 2023 na Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Akifafanua ajenda ya mkutano huo, Waziri Nchemba amesema nchi washiriki zitaweka nia ya pamoja ya kuongeza uwekezaji katika eneo la rasilimali watu ili kuongeza tija ya uzalishaji.

Mkutano huo ulioratibiwa na Benki ya Dunia, unafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika na Tanzania ikiwa ndiye mwenyeji wake.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya