ZINAZOVUMA:

“Nataka kucheza Real Madrid pekee”

Kylian Mbappe amesema ataendelea kusalia PSG mpaka mkataba wake utakapomalizika...

Share na:

Nyota wa Ufaransa na klabu ya Paris Saint Germain Kylian Mbappe amesema kuwa anataka kusalia katika klabu yake hiyo ili mwakani aende akacheze Real Madrid.

Kylian Mbappe alikataa ofa kubwa kutoka nchini Saudi Arabia akisema kuwa bado anatamani kuendelea kucheza mpira barani Ulaya.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amewaambia wasaidi wake ambao walifanya mahojiani na kituo kimoja cha televisheni na kusema kwamba Mbappe anataka kucheza tu Real Madrid ya Hispania.

Real Madrid na klabu ya PSG wamekuwa hawana mahusiano mazuri na klabu ya PSG ilikataa kumuuza mchezaji huyo kwenda Madrid.

Mkataba wa Mbappe unamalizika msimu ujao wa 2024 na kama PSG haitamuuza sasa basi ataondoka bure kwenda kuichezea Real Madrid jambo ambalo PSG hawalitaki pia.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,