ZINAZOVUMA:

Mwita Waitara atoka nje ya Bunge akilia.

Mbunge wa Tarime vijijini Mhe Mwita Waitara ametoka Bungeni huku...

Share na:

Mbunge wa Tarime vijijini Mwita Waitara amechukua uamuzi wa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kutoridhishwa na majibu ya Serikali Bungeni kuhusu fidia kwa Wananchi walio karibu na Mgodi wa Barrick North Mara.

Akijibu hoja, Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato amesema Mgodi wa Barrick North Mara ulionesha nia ya kutaka kuchukua baadhi ya maeneo ya vijiji vinavyozunguka mgodi huo, lakini baadhi ya Wananchi wakaamua kuongeza majengo harakaharaka maarufu kama ‘Tegesho’, ndipo mgodi ukaachana na maeneo hayo kwani hayaathiri utendaji wao wa kila siku.

Aidha Waitara akasema Machi 28, Waziri wa Madini alisema malipo ya fidia yatalipwa kabla ya mwezi wa sita lakini majibu yanayotolewa sasa ni ya kisiasa na yenye maumivu makubwa kwa watu wa Tarime.

Mbunge huyo akaamua kutoka nje ya Bunge na kusema kwa hisia kali kuwa wana Tarime wanamjua adui yao.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,