ZINAZOVUMA:

Mwanamke ahukumiwa kunyongwa Singapore

Mwanamke mmoja nchini Singapore ahukumiwa kunyongwa baada ya kukutwa na...

Share na:

Mwanamke mmoja nchini Singapore, Saridewi Djamani (45) anatarajiwa kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha gramu 30 za dawa za kulevya aina ya heroin mnamo 2018.

Hukumu hiyo inatokea ikiwa ni miaka 20 imepita tangu mwanamke ahukumiwe kunyongwa nchini humo ambapo bilionea wa Uingereza, Richard Branson, ameikosoa nchi hiyo akisema hukumu ya kifo sio kizuizi dhidi ya uhalifu akidai kuwa lalanguzi wadogo wa dawa za kulevya wanahitaji usaidizi.

Singapore ina baadhi ya sheria kali zaidi za kupambana na dawa za kulevya ambapo hukumu ya kifo inaweza kutumika kwa usafirishaji wa zaidi ya gramu 15 ya heroin na zaidi ya gramu 500 ya bangi.

Mashirika mbalimbali ya haki za binadamu yamelaani kitendo hicho na kusema kuwa ni kinyume na haki za kibinadaamu.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya