ZINAZOVUMA:

Mvua kubwa zaua 15 China

Shirika la habari la nchini China limeripoti vifo vya watu...

Share na:

Shirika la habari la serikali ya China Xinhua linasema watu 15 wamefariki na wengine wanne hawajulikani waliko kutokana na siku kadhaa za mvua kubwa huko kusini magharibi mwa China.

Vifo hivyo vilitokea katika mji wa Chongqing, ambako mvua zimesababisha mafuriko makubwa yaliyowalazimisha watu wengi kuhama makazi yao yaliyofurika maji na kuzoa magari na kuvunja madaraja.

Shirika la habari la Xinhua linasema mvua na mafuriko yamevuruga maisha ya watu zaidi ya 130,000.

Rais Xi Jinping ameagiza mamlaka husika katika ngazi zote za serikali kulipa suala hili kipaumbele kwa kuhakikisha usalama watu na mali.

Wizara ya fedha imetenga zaidi ya dola milioni 44 kwa ajili ya mfuko wa msaada wa dharura kwa ajili ya Chongqing na maeneo jirani.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya