ZINAZOVUMA:

Muswada mpya wapendekeza miaka 50 jela dhidi ya LGBTQ

Muswada unaooendekezwa dhidi ya watu wanaojihusisha mapenzi ya jinsia moja...

Share na:

Mswada unaopendekezwa dhidi ya wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya unataka watu hao kufungwa jela miaka 50 kwa kujihusisha na vitendo hivyo.

Mapendekezo hayo yamepewa jina la ‘Mswada wa Ulinzi wa Familia wa 2023’, rasimu ya sheria ambayo inayofadhiliwa na mbunge wa Homa Bay Town Peter Kaluma, unapendekeza kupiga marufuku ushoga, miungano ya watu wa jinsia moja na shughuli za kampeni zozote za LGBTQ.

Pia unalenga kupiga marufuku gwaride za mashoga, mikusanyiko na maandamano barabarani, na mavazi yanayounga mkono ushoga hadharani.

Wamiliki wa majengo yanayotumika kuendeleza shughuli za mapenzi ya jinsia moja watalipa faini ya dola 14,000 au watakabiliwa na kifungo cha miaka saba jela iwapo mswada huo utaidhinishwa.

Wiki iliyopita viongozi wa dini na baadhi ya mashirika ya kijamii wlifanya maandamano ya kupinga LGBTQ katika mji wa pwani wa Mombasa.

Maandamano hayo yalifanyika baada ya Mahakama ya Juu kutoa uamuzi wa kuruhusu usajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya LGBTQ.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya