ZINAZOVUMA:

Musk apendekeza malipo ya mwezi kwa watumiaji wa X

Mmiliki wa mtandao wa X Elon Musk amempendekeza kuwe na...

Share na:

Tajiri na mmiliki wa mtandao wa X ambao zamani ulifahamika kama ‘twitter’ Elon Musk amependekeza kuwa watumiaji wake wote waanze kulipia ili kupata huduma za mtandao huo.

Katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Musk alisema mfumo wa malipo ndiyo njia pekee ya kukabiliana na matumizi ya akaunti zinazoendeshwa na roboti.

“Tunaelekea kuwa na malipo madogo ya kila mwezi kwa matumizi ya mfumo,” Boss huyo alisema ambae ni mmiliki wa Tesla na SpaceX.

BBC ilitaka maeleo Zaidi kutoka kwa X kama kampuni lakini bado haijapokea taarifa rasmi mpaka sasa.

Haijulikani ikiwa mazungumzo hayo yalikuwa ni maoni tu ya pembeni au ni ishara ya mipango thabiti ambayo bado haijatangazwa.

Hata hivyo Musk amekuwa akisema kwa muda mrefu kuwa suluhisho lake la kuondoa roboti na akaunti feki kwenye jukwaa la mitandao ya kijamii ni kutoza ada kwa watumaiji wake.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,