Mamlaka nchini Ujerumani imekua ikipitia ukosoaji mkubwa kufuatia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha maafisa wa polisi wakimchukua mtoto mdogo wa kiislamu kwa lazima na kumtengenisha na familia yake.
Video hiyo imesambaa ikionesha maafisa hao wakiingia nyumbani kwa familia ya mtoto huyo na kutumia nguvu kumchukua huku akilia akiomba msaada.
Licha ya wanafamilia kuomba msaada na kusisitiza mtoto huyo asichukuliwe sababu ni mgonjwa hivyo hatakiwi kutengenishwa nao lakini haikua hivyo.
Polisi hao walisema maamuzi ya kumkamata mtoto huyo yametoka mahakamani na wao wametimiza maamuzi ya mahakama.
Jeshi la polisi nchini humo limethibitisha kutokea Kwa tukio hilo lakini limesema video hiyo imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwa nia ovu.