Mtandao wa twitter upo mbioni kubadili jina lake na kuzindua jina jipya litakalotumika ambalo pia litakuja na muonekano mpya wa mtandao huo.
Taarifa hiyo iliyotolewa na mmiliki wa Kampuni hiyo, Elon Musk ambaye amesema Twitter itaitwa ‘X’ na itapatikana kwa tovuti ya ‘x.com’, pia, ‘Logo'(nembo) ya ndege wa Blue itaondolewa rasmi na kuanza kutumika logo ya ‘X’.
Aidha, Musk amesema mwonekano wote wa Mtandao huo utakuwa umebadilika kufikia Julai 24, 2023, na hiyo ni endapo ataridhishwa na mwonekano wa mabadiliko hayo mapya.
Tangu alipoinunua kampuni hiyo kwa zaidi ya Tsh. Trilioni 102, Musk amefanya mabadiliko kadhaa ikiwemo kupunguza Wafanyakazi, Kubadili Mkurugenzi Mtendaji, mabadiliko ya baadhi ya Vipengele na kuanzisha kwa utaratibu wa kulipia ili kuwa na Alama ya Uthibitisho (Blue Tick)