ZINAZOVUMA:

MSD HAKIKISHENI VITUO VYA AFYA VINA DAWA

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa wilaya...

Share na:

Kaimu Mkuu wa mkoa wa Tanga ameitaka Bohari ya Dawa nchini MSD kuhakikisha vituo vyote vya afya mkoani humo, vinakuwa na dawa muhimu ili kupunguza malalamiko ya wananchi juu ya ukosefu wa dawa.

Mkuu wa wilaya ya Tanga, James Kaji ambaye alikuwa akikaimu Ukuu wa Mkoa aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa wadau wa MSD Kanda ya Tanga.

Ambapo alisema kuwa kutokana na uwekezaji wa serikali, ni muhimu kusiwepo na changamoto ya ukosefu wa dawa na vifaa tiba kwenye vituo.

“Serikali imeongeza bajeti ya afya hivyo ni jukumu la kuhakikisha mnasimamia bidhaa za afya, kwa kuzifikisha kwenye vituo vya kutolea huduma, ili kupunguza malalamiko ya wananchi ya ukosefu wa dawa wanapokwenda kupata matibabu” amesema Kaimu Mkuu wa mkoa .

Hata hivyo Mkurungenzi wa ugavi na uendeshaji kutoka MSD Makao Makuu Victor Sungusia, amesema kuwa bohari inaendelea na uboreshwaji wa huduma zake ili kuhakikisha huduma bora kwa wananchi inaendelea kutolewa.

Na Meneja wa Kanda ya Tanga Sitti Abdurahman amesema kuwa, kwa kushirikiana na Wizara ya afya wamekuwa wakihakikisha, vifaa vinavyohitajika vinapatikana na kusambazwa kwenye vituo vya afya.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya