ZINAZOVUMA:

HHRD yagawa vifaa tiba vyenye thamani ya milioni 650.

Taasisi ya 'Helping Hand for Relief and Development Africa' imegawa...

Share na:

Taasisi ya Helping Hand for Relief and Development (HHRD) tawi la Afrika imefanikiwa kugawa vifaaa vya afya vyenye thamani ya shilingi milioni 650 katika viwanja vya Maisara, mjini Zanzibar.

Ugawaji wa vifaa hivyo umelenga kuunga mkono juhudi za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuisaidia jamii ya Zanzibar kujikinga na kupambana dhidi ya maradhi.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ally Mwinyi, waziri wa Afya wa seikali ya mapinduzi ya Zanzibar, Mhe Ahmed Nassor Mazrui ameishukuru taasisi ya HHRD kwa kutoa msaada huo utakaoenda kuboresha utolewaji wa huduma za afya.

Aidha timu ya HHRD ikiongozwa na mwenyekiti wa bodi ya taasisi hiyo ndugu Yassir Salim Masoud na mwenyekiti Bwana Hassani Kimbwembwe imesema vifaa hivyo vitaongeza ufanisi wa huduma za afya lakini pia vitaenda kusambazwa katika hospitali za serikali zilizopo Zanzibar.

Kwa upande wa jamii iliyokuwepo kushuhudia ugawaji wa vifaa hivyo imeishukuru Helping Hand for Relief and Development Africa (HHRD) kwa kufanya wapate huduma za afya rahisi na kwa ufanisi kupitia vifaa walivyovitoa

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya