ZINAZOVUMA:

TMDA iongeze ufanisi kudhibiti dawa feki

Mamlaka Udhibiti wa Dawa na Vifaa tiba imetakiwa kuongeza ufanisi...

Share na:

Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Stanslaus Nyongo ameitaka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kuongeza nguvu ya kudhibiti bidhaa feki za dawa zinazoingia nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Nyongo ameyasema hayo leo Agosti 17, 2023 baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Bw. Adam Fimbo katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.

“Tunaona juhudi mnazofanya za kuteketeza dawa feki zinazoingia nchini, hii inaonesha bado kuna mianya mingi ya kuingiza dawa nchini hivyo ni muhimu sana kuongeza nguvu ya kudhibiti uingizwaji wa dawa feki”, amesisitiza Mhe. Nyongo

Aidha, Mhe. Nyongo ameitaka Mamlaka hiyo kuangalia ufanisi wa dawa zilizopo kwa maana kuna baadhi ya dawa hazina ubora mzuri unaotakiwa kulingana na dawa husika hasa kwenye dawa wa ‘Antibiotic’.

“Kuangalia ufanisi wa dawa iwe kipaumbele cha kwanza hasa kwenye hizi dawa za ‘Antibiotic’, maaana anaweza kuja mgonjwa anasema nikitumia dawa hii inaniponyesha kwa haraka kuliko nikitumia dawa hii, Sasa hii ni changamoto kwenu mkalifanyie kazi”, amesema Mhe. Nyongo

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya