Mke wa mchezaji wa klabu ya soka ya PSG, inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa (Ligue 1) na timu ya Taifa ya Morocco, Achraf Hakimi amedai talaka kutoka kwa mchezaji huyo na kutaka wagawane mali nusu kwa nusu. Hata hivyo mahakama imemwambia mwanamke huyo kwamba mume wake huyo ambae ni tajiri hana mali anayomiliki kwa jina lake, mali zake zote ameziandikisha kwa jina la mama yake mzazi.
Licha ya utajiri alionao na kulipwa Euro milioni moja kwa mwezi Achraf Hakimi katika mshahara wake asilimia 80 anaingiza katika akaunti ya mama yake. Inasemekana kuwa mali zote ikiwemo magari, nyumba na vitu vingine vya thamani vya mchezaji huyo vimeandikwa kwa jina la mama yake Bi Fatma na hata akitaka kununua kitu basi anamuomba mama yake ambae ndio humnunulia.