Licha ya onyo kutolewa na Raisi wa Kenya William Ruto lakini pia vyombo vya usalama nchini humo bado kumefanyika maandamano hii leo kama ilivyoelezwa hapo awali na wananchi wenye dhamira ya kuandamana.
Hata hivyo kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga alisema haogopi kutishiwa na kuwataka wananchi waungane mkono kuandamana.
Vyombo vya Ulinzi na usalama vilisema havitaruhusu na itakapobidi basi vitatumia vitoa machozi ili kuzuia maandamano hayo.
Mpaka sasa mtu mmoja ameuawa, miundombinu imeharibiwa na baadhi ya maeneo yamefungwa nchini Kenya kutokana na maandamano yanayoendelea yakipinga kupanda kwa gharama za maisha.
Hivi karibuni Rais William Ruto alisema wanaoendesha maandamano wanalenga kumpinga kwa sababu anataka kuwapatia vijana kazi.