ZINAZOVUMA:

Mlinzi binafsi wa Messi aingia uwanjani kumzuia shabiki

Mlinzi binafsi wa mchezaji Lionel Messi ameingia uwanjani kumlinda mchezaji...

Share na:

Shabiki mmoja nchini Marekani amejaribu kuingia uwanjani ili kwenda kukutana na mchezaji Lionel Messi wakati mchezo ukiwa unaendelea.

Shabiki huyo hakufanikiwa adhma yake baada ya mlinzi binafsi wa Nyota huyo kuwahi na kumzuia na kumuondoa uwanjani.

Vidio inayosambaa mitandaoni inamuonesha mlinzi binafsi wa Messi akimuwahi shabiki huyo kabla hajamkumbatia.

Tukio hilo limetokea wakati wa mchezo kati ya Inter Miami na klabu ya LAFC katika kipindi cha pili cha mchezo.

Mlinzi binafsi wa Messi alietambulika kwa jina la Yassine Chueko amekuwa maarufu hivi karibuni baada ya kuonekana kila sehemu ambayo Lionel Messi yupo.

Mlinzi huyo husimama pembezoni mwa uwanja na hutembea sawa na Messi anavyotembea akiwa uwanjani.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya