ZINAZOVUMA:

“Miradi ya Uviko 19 ipo chini ya kiwango” CP. Salumu Hamduni

Raisi Samia amepokea ripoti ya TAKUKURU ya 2021/2022 ambayo imegundua...

Share na:

Raisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani leo tarehe 29 March 2023 amepokea ripoti ya TAKUKURU ya mwaka 2021/2022 kutoka kwa CP. Salumu Hamduni ambae ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU).

Katika ripoti hiyo Salumu Hamduni amesema kuna baadhi ya mapungufu yalionekana katika utekelezaji wa miradi ya Uviko 19.

Mapungufu hayo ameyataja ikiwa ni pamoja na ubora wa kazi usioridhisha, Sheria za Manunuzi ya umma kutokuzingatiwa, michakato ya zabuni kuanzishwa bila uwepo wa vigezo, lakini pia ununuzi wa bidhaa Kwa bei kubwa wakati bei ndogo zipo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya