ZINAZOVUMA:

Mgogoro Niger, Ufaransa yaonywa

Burkina Faso pamoja na Mali zimetoa onyo kwa Ufaransa kutoingilia...

Share na:

Uongozi mpya wa kijeshi nchini Niger umeishutumu Ufaransa kutaka kuingilia kati na kumrejesha madarakani Rais aliyepinduliwa Mohammed Bazoum.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Catherine Colonna bado wanaamini kuwa inawezekana kumrejesha madarakani Bazoum.

Hata hivyo nchi za Mali na Burkina Faso zinazoongozwa kijeshi zimeingilia kati pia zikiitetea Niger na kuonya kwamba nchi yoyote itakayoingilia kati kinachoendelea Niger basi itakua sawa na kutangaza vita na nchi hizo mbili.

Bazoum ni mshirika wa karibu wa nchi za magharibi ambaye kuchaguliwa kwake miaka miwili iliyopita kuliashiria kukabidhiana madaraka kwa njia ya amani kwa mara ya kwanza tangu uhuru wa Niger, aliondolewa madarakani tarehe 26 Julai na kiongozi wa kikosi cha ulinzi wa rais.

Mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Rais Jenerali Abdourahamane Tiani alijitangaza kuwa kiongozi, lakini madai yake yalilaaniwa kimataifa, na Jumuia ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ilimpa wiki moja kurudisha madaraka.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya