Kampuni META inayomiliki Mitandao ya Kijamii ya Facebook, Instagram na WhatsApp imezundua ‘App’ nyingine ya Kijamii inayoelezwa kuwa itakuwa mshindani wa Twitter.
Mkurugenzi Mkuu wa META Mark Zuckerberg amesema kuna kitu Twitter walipaswa kufanya na hawajakifanya hivyo ‘Threads’ inakuja kwaajili hiyo, japo itachukua muda kuifikia Twitter lakini Mtandao huo unalenga kuhudumia zaidi ya Watu Bilioni 1.
META imeeleza kuwa ‘Threads’ haitopatikana kwenye Nchi za Umoja wa Ulaya kwa sasa, na pia itaruhusu Mtumiaji kuchapisha ujumbe wenye maneno 500 pia una vitu vingi vinavyofanana na Twitter.
Hata hivyo, Watumiaji wameonesha wasiwasi wao kuhusu kiwango cha ‘TaarifaBinafsi zinazokusanywa na ‘Threads’ zikiwemo Taarifa za Afya, Fedha na nyingnezo, zote zikiwa na uhusiano na Utambulisho wa Watumiaji.