ZINAZOVUMA:

Messi kurudi Barcelona

Raisi wa Barcelona Joan Laporta amesema klabu hiyo ipo tayari...

Share na:

Rais wa Barcelona Joan Laporta amesema klabu hiyo ipo tayari kumrejesha Lionel Messi kwani Barcelona ndio nyumbani kwa Messi.

Klabu ya Barcelona inatarajia kumsajili tena fowadi huyo msimu huu wa joto ambapo anatarajiwa kumaliza mkataba wake na timu yake ya sasa Paris Saint Germain PSG June 30 mwaka huu.

Hata hivyo tetesi zinamuhusisha sana nyota huyo wa Argentina kuwa huenda akatimkia nchini Saudi Arabia na kwenda kulamba dili nono sana.

Lakini katika mahojiano na shirika la utangazaji la Uhispania TV3, Laporta alisema Barcelona inaweza kushindana na mtu yeyote kuwania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35.

Messi aliondoka kwa wababe hao wa Hispania miaka miwili iliyopita baada ya kucheza kwa miaka 21 katika klabu hiyo lakini amekuwa na wakati mgumu katika misimu yake miwili nchini Ufaransa, huku ikifikia hatua mashabiki kumzomea.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya