Mchezaji wa PSG na timu ya Taifa ya Argentina Lionel Messi ameomba radhi kwa klabu yake na wachezaji wenzake baada ya timu yake kumpa adhabu ya kumsimamisha kwa wiki mbili.
Adhabu hiyo ilitokana na yeye kuondoka kambini kwenda kwenye biashara zake binafsi nchini Saudi Arabia bila ruhusa ya timu.
Nyota huyo ameomba radhi licha ya kuwa amebakisha muda mchache wa kuendelea kuitumia klabu hiyo huku ikifahamika kuwa hatoongeza mkataba mwingine baada ya mkataba wake kutamatika June 30, 2023.
Lionel Messi amesema anahitaji kucheza katika mechi ambazo zimebakia akiwa na timu yake hiyo, wadau mbalimbali wamempongeza mchezaji huyo kwa nidhamu kubwa aliyoionesha kwa kuomba radhi hadharani.