ZINAZOVUMA:

Melinda gates ajiuzulu uenyekiti wa gates Foundation

Bi. Melinda gates ajiuzulu nafasi ya mwenyekiti mwenza katika Shirika...

Share na:

Bi Melinda Gates aliyekuwa mke wa Bill Gates na pia mwenyekiti mwenza katika asasi ya Gates Foundation, ametangaza kijiuzulu nafasi ya mwenyekiti katika taasisi hiyo kubwa ya misaada duniani.

Taarifa hiyo ya kujiuzulu kwake ilitolewa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X sik ya Jumatatu, na kusema kuwa Juni 7 ndio itakuwa siku yake ya mwisho katika taasisi hiyo.

Melinda na Mumewe Bill Gates walianzisha taasisi hiyo ya Gates Foundation wakati huo ikiitwa Bill and Melinda gates Foundation mwaka 2000.

Mwaka elfu 2021 waliachana na mumewe, ila waliahidi kundelea kufanya kazi pamoja katika taasisi hiyo ya Gates Foundation.

Taasisi hiyo tangu kuanzishwa imekuwa ikitoa huduma ya afya kwa kutoa misaada mbalimbali ya kiafya katika nchi nyingi duniani.

Katika taarifa hiyo ya kujiuzulu amesema mengi kwa hisia kama “haikuwa rahisi kufikia uamuzi huu” na “Najivunia sana taasisi ambayo mimi na Bill tuliijenga pamoja,”.

Katika kuendeleza juhudi zake za kusaidia jamii Bi Melinda Gates alianzisha Pivotal Ventures kama kampuni ya uwekezaji ili kusaidia wanawake na familia.

Kampuni hiyo inalenga kuondoa vikwazo vya fursa kwa wanawake na vikundi vya walio wachache (Minorities).

Anatarajia kuwa anaweza kupata Dola Bilioni 12.5 kwa ajili ya kuendeleza kazi zake za uwekezaji katka kampuni ya Pivotal Ventures.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,