ZINAZOVUMA:

Mchengerwa: halmashauri biashara ya hewa ukaa inalipa

Waziri wa TAMISEMI awataka wakurugenzi wa wilaya wenye misitu ya...

Share na:

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa, amewataka wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ambao maeneo yao kuna misitu ya asili kuanzisha biashara ya hewa ukaa kama chanzo kipya cha mapato.

Alisema hayo leo alipokuwa akifunga kikao cha siku tatu na Wakurugenzi hao, kilichofanyika shule ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo kibaha mkoani Pwani.

Amesema biashara ya hewa ukaa (Carbon Credit) ni biashara mpya na inafanya vizuri sana kwenye baadhi ya Halmashauri, mfano mzuri Halmashauri ya Tanganyika na ni chanzo kizuri cha mapato na cha uhakika.

“Sasa nizitake halmashauri nyingine zenye misitu kuhakikisha wanaanza biashara hii mara moja, ninawapa mwezi mmoja mkajifunze Halmashauri ya Tanganyika ambao wameshafika mbali kwenye Biashara hii”

Halmashauri ya Tanganyika ni jina jipya, na hapo mwanzo ilikuw wilaya ya Mpanda, iliyopo katika mkoa wa Katavi.


“kwa mwaka Halmashauri ya Tanganyika wanapata Sh. Bilioni 14, ambazo zinasaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, hivyo na nyie mkajifunze muone namna ya kuanza biashara hii ili kuongeza mapato ya Halmashauri zenu.”

“Mtakumbuka kuwa wiki mbili zilizopita wakati nafungua Mkutano wa 38 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania, niliwaelekeza kila Mkurugenzi kuhakikisha ameanzisha vyanzo vipya viwili vya mapato sasa niwape chanzo cha kuanza nacho ni hiki cha hewa ukaa,”amesema.

Aidha,katika mambo yaliyosisitizwa na Mchengerwa kwa wakurugenzi ni kwenda kusimamia ajenda ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kutumia mashine za kieletroniki pamoja na matumizi sahihi ya mapato hayo hususani ni kwenye miradi ya maendeleo.

“Mapato na damu ya maendeleo bila mapato hakuna maendeleo, bado hamfanyi vizuri kwenye eneo hili, nendeni mkakusanye mapato kikamilifu na mtumie mifumo ipasavyo katika zoezi zima la ukusanyaji, matumizi ya mifumo ya kielektroniki yameonyesha mafanikio makubwa na ufanisi katika ukusanyaji wa fedha za Serikali,”amesema.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya