ZINAZOVUMA:

Marekani yawawekea vikwazo maafisa kutoka Mali

Marekani imetangaza kuwawekea vikwazo maafisa wa Jeshi la Mali kwa...

Share na:

Marekani imetangaza kuweka vikwazo dhidi ya maafisa wakuu watatu kutoka nchini Mali wanaosemekana kuratibu kuenea kwa kikundi cha kijeshi cha Urusi cha ‘Wagner’ katika nchi hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken huku akiwataja maafisa hao ambao ni Waziri wa Ulinzi wa Mali, Mkuu wa Jeshi la Anga na Naibu Mkuu wa Majeshi.

Anthony Blinken anasema vifo vya raia vimeongezeka kwa zaidi ya mara tatu tangu vikosi vya Wagner kutumwa Mali mnamo Desemba 2021, akiongeza.

“Wingi waa vifo hivyo vilitokana na operesheni zilizofanywa na wanajeshi wa Mali pamoja na wanachama wa kundi la Wagner”. Aliongeza

Marekani na washirika wake kwa miaka kadhaa wameliwekea vikwazo kundi la Wagner na wafuasi wake, wakilishutumu kundi hilo la kijeshi kwa ukiukaji wa haki na kueneza habari potofu.

Itakumbukwa pia mapema Januari, Marekani ililitaja kundi la Wagner kama shirika la uhalifu la kimataifa.

Wiki iliyopita, Uingereza iliwawekea vikwazo pia watu 13 wenye uhusiano na Wagner katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Mali na Sudan.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya