ZINAZOVUMA:

Marekani yaingiza nchini mchele wenye virutubisho

Marekani yaingiza nchini mchele na majaragwe yaliyoongezwa virutubisho kwa shule...

Share na:

Wizara ya Kilimo ya Marekani, kwa ushirikiano na Jumuiya za Kimataifa, imetoa msaada wa kwanza wa mchele ulioongezwa virutubisho, maharage na mafuta ya alizeti kutoka kwa wakulima wa Marekani moja kwa moja hadi shuleni katika eneo la Dodoma nchini Tanzania.

Msaada huo umetolewa chini ya mpango unaoitwa “Pamoja Tuwalishe” ambao umekusudia kutoa milo yenye lishe kwa wanafunzi katika shule zaidi ya 300 zinazoshiriki, pia wataanzisha bustani za shule, na kujifunza mbinu za kuvuna maji ya mvua.

Kwa mujibu wa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, programu hiyo inaakisi ahadi na dhamira yao ya dhati ya kukuza afya, elimu, na fursa kwa watoto kote ulimwenguni.

Nini maoni yako katika jambo hili?

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya