ZINAZOVUMA:

Mandonga ruksa kupanda ulingoni

Bondia Karim Mandonga ameruhusiwa kuendelea na mapambano yake yanayofata baada...

Share na:

Bondia maarufu nchini Tanzania Karim Mandonga ameruhusiwa kuendelea na mapambano yake yanayofata baada ya uchunguzi kubaini kuwa hajaathirika maeneo aliyofanyiwa uchunguzi.

Hivi karibuni Mandonga alisimamishwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini Tanzania ili kupisha uchunguzi wa kitabibu wa afya yake baada ya kupoteza kwa Technical Knock Out (TKO) katika mapambano yake mawili ya mwisho.

Matokeo ya uchunguzi wa kitabibu yaliyofanyika yametoa majibu kuwa Mandonga hajaathirika katika maeneo yaliyofanyiwa uchunguzi na kuruhusiwa kuendelea na mapambano yake yanayokuja hivi karibuni.

Mandonga anatarajiwa kuingia ulingoni tarehe 27 mwezi huu huko Zanzibar na amesema yupo vizuri na anajiandaa na pambano hilo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya