ZINAZOVUMA:

Mama lishe Jela kwa kuishi kinyumba na mtoto

Mtwara: Mama lishe afungwa miaka 15 kwa kuishi kinyumba na...

Share na:

Mfanyabiashara ndogondogo ya kuuza chakula maarufu kama “Mama lishe” Asha Chamchuno (46) amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumnyanyasa kingono mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 15.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mtwara, Issa Suleiman alisema mamalishe huyo alikutwa akiishi kinyumba na mtoto huyo, na kuendelea kusema kwa waandishi kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Machi 22, mwaka huu.

Katika kesi nyingine Kamanda Suleiman alisema watu watatu wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kulawiti, kumpiga picha mwathirika wakati wakimlawiti, kurekodi video na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Aliwataja waliohukumiwa kuwa ni Shabibu Said aliyekuwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na wezake watatu.

Alisema awali washtakiwa walihukumiwa kulipa faini ya Sh 1,000,000 katika Mahakama ya Wilaya ya Mtwara.

Kamanda Suleiman alisema baadaye upande wa Jamhuri ulikata rufaa Mahakama Kuu, Kanda ya Mtwara na rufaa hiyo ilisikilizwa Aprili 3, mwaka huu.

Mahakama Kuu ilibatilisha adhabu ya faini na kutoa kifungo cha miaka 30 jela kwa washitakiwa hao na wameanza kutumikia adhabu hiyo.

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,