Barabara Kuu ya kwenda mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara) imeharibika maeneo ya Somanga, ambapo kipande cha barabara kimesombwa na maji usiku wa jana.
Watu wa eneo hilo wanasema kuwa jana mchana mvua kubwa imenyesha maeneo ya bonde hilo, na kusababisha kusombwa kwa daraja la Somanga Mtamba jioni ya jana.
Hali iliyosababisha kukosekana kwa mawasiliano ya ardhi baina ya mikoa ya Kusini na Dar es Salaam kwa njia hiyo.
Na watu wengi wa maeneo hayo jirani wameathirika kwa mafuriko na wengine wakiwa na majonzi kwa kutokujua hali za ndugu zao.
Tayari kuna hatua za dharura zimechukuliwa na mkandarasi YiSheng Construction anaendelea na ukarabati wa daraja hilo.
Pia juhudi za uokoaji zimefanyika tangu jana kwa wale walioathirika na mafuriko wakazingirwa na maji maeneo hayo. Na kuna baadhi ya watu waliokolewa jana.
Taarifa zaidi
Na baada ya kazi ya haraka iliyofanywa na mkandarasi Yisheng Construction tayari magari yameruhusiwa kupita eneo hilo kuanzia majira ya mchana wa leo tarehe 25 Machi 2024.