Mahakama Kuu nchini Zimbabwe imewaondoa Wagombea 12 wa Ubunge kutoka Chama kikuu cha upinzani nchini humo (CCC) kushiriki katika uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mwezi wa nane.
Mahakama imesema kuwa wagombea hao wameondolewa kwa kigezo cha kuwa maombi yao yaliwasilishwa baada ya muda stahiki wa kupokea maombi.
Uamuzi huo unamaanisha kuwa Wagombea wa Chama tawala cha Zanu-PF watapita bila kupingwa katika Majimbo Matatu Mjini Bulawayo, ambao hapo awali ulikuwa ngome ya Upinzani.
Wananchi wa Zimbabwe watapiga kura tarehe 23 Agosti 2023 kuwachagua Madiwani, Wabunge na Rais