ZINAZOVUMA:

Mabasi ya Umma yasitisha huduma Kinshasa

Wakazi wa Kinshasa wapata kero ya usafiri kutokana na mafuta,...

Share na:

Mji mkuu wa DRC, Kinshasa, unabeba mzigo mkubwa wa kutokuwepo kwa mabasi kutoka kwa kampuni ya usafiri wa umma (Transco).

Kufuatia tatizo la ugavi wa mafuta ya serikali, kampuni inayosafirisha wakazi wa Kinshasa kwa bei nafuu inatatizika kwa shughuli ya usafirishaji wa watu. Suala hilo lilijadiliwa mwisho wa wiki iliyopita katika kikao cha baraza la mawaziri nchini humo, bila kutatua mgogoro huo.

Wateja walipata kero siku ya Jumatatu huku msururu wa watoto wa shule wakisubiri mabasi ya kampuni hiyo ilionekana kwenye barabara za mji huo asubuhi, wakati watumishi wa umma wakijazana kwenye mabasi ya watu binafsi.

Hali hiyo ni neema kwa waendesha pikipiki za kukodi “bodaboda” ambazo zimenufaika kwa kuongeza maradufu bei ya nauli.

Kampuni ya Transco imekosa mafuta kwa ajili ya mabasi yake, wakati huo huo Serikali hulipa karibu dola milioni 1 kila mwezi kwa kampuni kama ruzuku ya mafuta na vipuri.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya