ZINAZOVUMA:

Mabadiliko Baraza la Mawaziri ni sawa na mabadiliko ya timu mpira

Spika wa Bunge Dkt Tulia Akson amesema Mawaziri ambao hawajachaguliwa...

Share na:

Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson amewataka mawaziri waliopumzishwa katika Baraza la Mawaziri wasiwe na wasiwasi, kwani hiyo ni hali ya kawaida ni kama kocha katika timu za Simba na Yanga anapofanya mabadiliko ya kikosi chake kutegemea na mechi iliyo mbele yao.

Akizungumza bungeni leo wakati akitoa salamu za pongezi kwa Naibu Waziri Mkuu, Dkt Dotto Biteko, Spika Tulia amesema wapo mawaziri ambao walipumzishwa na baadaye wakarejeshwa katika baraza, hivyo hilo ni suala la kawaida.

Spika Dkt Tulia amesema bunge litaendela kuwapa ushirikiano mawaziri na manaibu ambao wameendelea kuaminiwa, pamoja na wapya.

“Na wale ambao mmepumzika kidogo msiwe na wasiwasi, hili baraza lina watu ambao waliwahi kupumzika, wakarejea, wakapumzika tena, wakarejea,” amesema na kuwataka wasiwe na wasiwasi kwani nafasi hizo ni kwa zamu.

“Mtu zamu yake inafika basi anapewa kufanya hiyo kazi, zamu yake inapopungua kidogo ni kama kocha anaweka huyu si kwamba wewe uliyetoka ni mbaya ama namna gani, bali kocha anataka kukupumzisha kwa ajili ya maandalizi ya shughuli nyingine hapo baadaye,” amesema Spika.

Ametolea mfano kama wa timu za Simba na Yanga, zinapoamua kupumzisha wachezaji wao kwa ajili ya mechi fulani ngumu iliyo mbele yao

Endelea Kusoma

Vyombo vya Habari nchini Iran vimeanza kutangaza kifo cha Rais Ebrahim Raisi,