ZINAZOVUMA:

Maadhimisho ya miaka 30 ya MTP yafana

Msaud Tuition Program (MTP) imefanya maadhimisho ya miaka 30 tangu...

Share na:

Taasisi ya Msaud Tuition Program MTP Jana Agosti 27, 2023 imefanya maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwake ambayo yalifanyika katika ukumbi wa DYCCC Yemen Changombe, Dar es salaam.

MTP imekua ikiwasaidia wanafunzi wa kiislamu kwa miaka yote 30 kuwapa elimu katika muda wa ziada nje na ule wa shule ili kuhakikisha wanafanya vzuri na kutengeneza jamii ya wasomi.

Maadhimisho hayo yalilenga kuwakutanisha pamoja wadau wote wa MTP kuanzia waanzilishi, wanafunzi wa mwanzo, walimu wa MTP pamoja na wanafunzi wa sasa ambao wanaendelea kunufaika na MTP.

Miongoni mwa mengi yaliyozungumzwa katika maadhimisho hayo ni pamoja na kuanzisha kituo cha ubora ‘Centre of Excellence’ ambacho kitatumika kuwakutanisha pamoja wadau wote wa MTP.

Aidha Mgeni rasmi Mhe. Ansar Kachwamba alizindua rasmi harambee ya kuichaingia MTP ili kuweza kupata pesa za kujiendesha katika shughuli zake.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya