ZINAZOVUMA:

LHRC yakemea watu kutishiwa maisha

Kituo cha sheria na haki za binadamu kimekemea vitendo vya...

Share na:

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimekemea vikali matukio ya kutishiwa maisha kwa baadhi ya Watanzania wanaoonekana kuwa na mlengo au maoni tofauti.

Sambamba na hilo, LHRC imekemea vitendo vya baadhi ya viongozi wa Serikali hususani mawaziri kutoa maonyo ambavyo yanaashiria kuwatishia Watanzania wanaotekeleza uhuru wao wa kutoa maoni kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamli.

Katika taarifa ya kituo hicho iliyotolewa jana Julai 10, 2023 imeeleza kuna malalamiko ya watu wanaotishiwa maisha yao na watu wasiojulikana kwa sababu maoni yao yanakinzana na yale ya upande mwingine hasa kwenye mijadala inayohusu maslahi mapana ya Taifa.

“Uhuru wa kujieleza unalindwa na kuhifadhiwa kwa mujibu Ibara ya 19 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa wa Mwaka 1966, Ibara ya 9 ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu wa mwaka 1989, ambapo Tanzania ni nchi mwanachama wa mikataba hii mtawalia.

“Wakati huo huo uhuru wa kujieleza unalindwa na kuhifadhiwa na Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kadhaa,” imeeleza taarifa hiyo.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya