Klabu ya soka ya Simba imetangaza kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Assec Mimosa ya Ivory Coast, Aubin Kramo kwa mkataba wa miaka miwili.
Aubin Kramo Kouame (27) raia wa Ivory Coast, anamudu kucheza nafasi ya winga wa kushoto na anajiunga na Simba SC akitokea Assec Mimosa alipohudumu kwa misimu miwili tangu August 2021 alipojiunga nayo akitokea FC San Pedro.
Kramo alikuwa sehemu ya kikosi cha Assec Mimosa kilichofika hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Africa na kuifungia klabu yake hiyo ya zamani magoli manne (4).