Shirika la ndege la Kenyan Airways (KQ) limetaja upepo mkali kama sababu ya ndege yake, kushindwa kutua katika uwanja wa kimataifa wa Aden Adde wiki moja baada ya tukio jijini Mogadishu.
Na kuongeza kuwa marubani hawakutaka kuchukua hatua nyingine ili kungoja mamlaka ya uwanja kushughulikia changamoto hiyo ya kiusalama waliyoyaona.
Shirika hilo katika taarifa yake hiyo lilisema kuwa mamlaka jijini Mogadishu zimesha shughulikia suala hilo na wataweza kutua kwa usalama.
Ingawa shirika hilo la KQ halikuweka wazi ni ndege ngapi zilirudishwa kutoka Mogadishu, na hawakusema pia kwa nini waliendelea kupeleka ndege Mogadishu wakati changamoto hiyo ikiwa haijatatuliwa.
Pamoja na taarifa hiyo uchambuzi wa taarifa mbalimbali umeonesha ndege za mashirika mengine zimetua katika uwanja huo nchini Somalia bila matatizo kama ndege ya Kenyan Airways.