ZINAZOVUMA:

OCHA Somalia: Mvua hizi zitaathiri watu laki 7 nchini

Ofisi ya Umoja wa Mataifa za kuratibu Masuala ya Kijamii...

Share na:

Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) ilisema Jumapili kwamba mvua kubwa zaidi zinazotarajiwa kunyesha zikiambatana na mafuriko katika wilaya 22 za Somalia zitaathiri takriban watu 770,000.

OCHA ilisema mvua hizi zijulikanazo kama Gu zinazoanzia Aprili hadi Juni zimeanza katika mikoa mingi nchini humo huku katika baadhi ya maeneo ikinyesha mvua kubwa, lakini hakuna mafuriko au mito iliyoripotiwa kufurika.

Katika taarifa yake mpya iliyotolewa mjini Mogadishu, nchini Somalia ofisi hiyo ilisema watoa misaada ya kibinadamu wameandaa mpango wa kupunguza athari zinazotarajiwa za mvua za Gu, lakini wanahitaji rasilimali za haraka ili kuhakikisha wanashughulikia kwa wakati.

Kwa mujibu wa OCHA boti 51 zipo kwa ajili ya kuwahamisha watu na kutoa usaidizi katika maeneo ya kipaumbele kando ya mito Shabelle na Juba, na pia kupeleka msaada katika maeneo yasiyoweza kufikika na kuwahamisha watu ambao wanaweza kukwama.

Hata hivyo OCHA ilisema mvua hizo zimeleta ahueni kwa wafugaji na wakulima kote nchini, kuzalisha malisho na kujaza maeneo ya maji.

Endelea Kusoma

Kijana Edward awebwa ahukumiwa miaka 6 jela nchini Uganda, kwa kumtukana rais

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya