ZINAZOVUMA:

kituo cha redio chafungiwa Burkina Faso

Burkina Faso imefungia moja ya redio nchini humo kwa kufanya...

Share na:

Serikali ya kijeshi nchini Burkina Faso imesitisha shughuli za moja ya redio maarufu nchini humo kutokana na redio hiyo kufanya mahojiano yanayodaiwa kudharau viongozi wapya wa jeshi katika nchi jirani ya Niger.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mawasiliano nchini Burkina Faso, Rimtalba Jean Emmanuel Ouedraogo amesema redio Omega imezuiwa mara moja kuendelea na shughuli zake kwa kipindi cha muda usiojulikana.

Redio hiyo ambayo ni sehemu ya kampuni ya mawasiliano ya Omega inayoomilikiwa na mwanahabari wa zamani Alpha Barry, imesitisha shughuli zake baada ya agizo hilo.

Kituo hicho kilikuwa kimefanya mahojiano na Ousmane Abdoul Moumouni, msemaji wa kundi jipya nchini Niger linalotaka kurejeshwa madarakani kwa rais Mohamed Bazoum.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya