ZINAZOVUMA:

Kiongozi wa Mwenge: Takukuru waleeni watoto wakatae rushwa

TAKUKURU waagizwa kuwalea watoto kuanzia ngazi ya shule ya Msingi...

Share na:

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa, Godfrey Mnzava ameiagiza Taasisi ya Kupambana na kuzuia Rushwa (TAKUKURU), kuwekeza kwa wanafunzi kuanzia ngazi za shule za msingi hadi sekondari kutambua athari za rushwa na kuwa zinakwamisha kupatikana kwa haki zao.

Agizo hilo amelitoa leo wakati wa kukagua na kufungua mradi wa vyumba vitano vya madarasa pamoja na ofisi ya walimu sambamba na klabu ya wapinga rushwa (TAKUKURU) katika shule ya Msingi Shashui iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli, mkoani Tanga.

Amesema kuwa kada hiyo ya watoto wadogo inategemewa kuja kuwa viongozi watakaotumikia taifa hili, hivyo ni muhimu waelimishwe madhara ya rushwa kuwa yanachangia kuwanyima haki zao na kurudisha nyuma maendeleo.

“TAKUKURU tusaidie kuwawezesha watoto wa Taifa hili watambue kuwa, rushwa ni kitendo cha kukiuka maadili na ni kitendo kibaya, hivyo wataweza kuchukia toka wangali watoto na tunaweza kuwa na Taifa ambalo linapohuru na vitendo vya rushwa “amesema kiongozi huyo.

Mwenge wa uhuru upo wilayani Bumbuli ambapo unatarajiwa kukagua, kuweka mawe ya msingi sambamba na kuzindua miradi ya maendeleo nane yenye thamani ya Sh bilioni 2.1.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya