ZINAZOVUMA:

Kilichojificha kupotea maafisa wa ngazi za juu China

Kumekua na muendelezo wa kupotea kwa maafisa mbalimbali wa ngazi...

Share na:

Kutoweka kwa maafisa wa ngazi za juu nchini China katika miezi ya hivi karibuni kumezua taharuki na maswali kipi kilichojificha nyuma yake.

Maswali yameelekezwa kwa Rais Xi Jinping kuwa huenda ameanza zoezi la kuwasafisha kwa kuwaondoa kutokana na tuhuma za rushwa.

Mtu wa hivi karibuni aliyetoweka ni Waziri wa Ulinzi Li Shangfu ambae hajaonekana hadharani kwa wiki kadhaa sasa. Awali kutoonekana kwake lilionekana ni jambo la kawaida lakini maswali yalizidi pale mwanadiplomasia wa Marekani alipobainisha hilo.

Ripoti ya Reuters baadaye ilisema Jenerali Li, aliyekuwa akisimamia ununuzi wa silaha kwa Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China (PLA) anachunguzwa kuhusu ununuzi wa vifaa vya kijeshi.

Kutoweka kwake kunakuja wiki kadhaa baada ya maafisa wawili wakuu wa kitengo cha kijeshi kinachosimamia makombora ya nyuklia na jaji wa mahakama ya kijeshi kutumbuliwa.

Hakuna maelezo mengi kuhusu kutumbuliwa huko mbali na kuelezwa kuwa ni sababu za kiafya japo kumekua na uvumi kwamba mamlaka inadhibiti ufisadi katika jeshi.

Uvumi umeenea pia kuwa baadhi ya makada wa Chama cha Kikomunisti cha China (CCP) kutoka kamati ya kijeshi inayodhibiti vikosi vya jeshi pia wanachunguzwa.

Aidha Jeshi limekuwa katika hali ya tahadhari kutoka mwezi Julai na ilitoa wito usio wa kawaida kuwataka wananchi kutoa taarifa kuhusu rushwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Endelea Kusoma

Mfalme Salman wa Saudi Arabia aongoza kikao cha baraza la Mawaziri baada

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya