Leo Mei 2, 2023 wanafunzi wa kidato cha sita kote nchini wameanza rasmi mtihani wao wa kuhitimu kidato cha sita (ACSEE 2023).
Serikali na wadau wa elimu mbalimbali wamewatakia kila la kheri vijana wote wanaoingia katika mitihani hiyo ya kumaliza elimu ya sekondari.
Upande wa serikali pia Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani ametuma salamu za kheri kwa wanafunzi hao
“Nawatakia kila la kheri wanangu wote mnaoanza mitihani yenu ya Kidato cha Sita kesho. Tunawategemea. Tunawaamini”.
“Naamini mmejiandaa vyema kwa hatua hii muhimu kwenye safari yenu ya elimu, na nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape utulivu na siha njema mkahitimishe salama na kwa mafanikio”.
“Serikali itaendelea kuhakikisha inaandaa mazingira bora katika safari yenu kuelekea hatua zifuatazo ikiwemo Vyuo vya Ufundi, Vyuo vya Kati na Vyuo vya Elimu ya Juu”.