ZINAZOVUMA:

Kesi za kubambikiwa bado zipo tendeni haki

Raisi wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassani amelitaka jeshi la...

Share na:

Rais Samia Suluhu Hassani amelitaka jeshi la polisi kuhakikisha linatenda haki Kwa watu wanaoamatwa na kufikishwa vituoni wawe kweli wanamakosa na sio kuwakomoa.

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumatatu Septemba 4, 2023katika hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika Oysterbay jijini Dar es Salaam.

“Bado napokea vikaratasi vya tatizo la
kubambikiwa kesi kwenye vituo vya polisi ambalo nalo naomba sana mlitupie macho, ili wale wanaopelekwa basi wawe na makosa ya kweli na sio ya kukomoana.

“Wananchi pia wanalalamika nasi tunayasikia hatuna budi kuyaleta kwenu ili yaweze kufanyiwa kazi”.

Aidha Rais Samia amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura kuhakikisha askari polisi wanakuwa na utimamu wa mwili ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya