ZINAZOVUMA:

Kesi ya Trump yapelekwa mbele mpaka Machi 4, 2024

Kesi inayomkabili Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump imepelekwa...

Share na:

Kesi ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump imepelekwa mbele na sasa itasikilizwa tena kuanzia Machi 4, 2024 katika mahakama ya shirikisho mjini Washington.

Maamuzi hayo yalitolewa na Jaji atakaeiongoza kesi hiyo Tanya Chutkan, siku ya Jana jumatatu Agosti 28 wakati wa kikao cha mapendekezo kutoka Katika pande zote mbili.

Mwendesha Mashtaka Maalum Jack Smith alitaka kesi ya Donald Trump ianze Januari 2, 2024 huko Washington lakini Jaji Tanya Chutkan amesema ni muda mfupi sana kujitayarisha.

Hata hivyo upande wa utetezi wa Donald Trump bado umeona muda huo ni mapema sana na kutaka kesi kusogezwa mbele mpaka mwezi Aprili 2024.

Donald Trump anatuhumiwa kwa majaribio yake ya kupanga njama za kuharibu uchaguzi wa Marekani wakati akichuana na Rais wa sasa Joe Biden.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya