ZINAZOVUMA:

Kenya yasimamisha mradi wa ‘WorldCoin’

Serikali nchini Kenya imetangaza kuusimamisha shughuli zote zinazofanywa na mradi...

Share na:

Serikali ya Kenya imesitisha shughuli zote zinazohusiana na mradi wa sarafu fiche za kidijitali wa ‘WorldCoin’.

Waziri wa Usalama wa Ndani nchimi humo Kithure Kindiki amesema kupitia taarifa iliyotolewa kwamba serikali ina wasiwasi kuhusu mradi huo ambao kufikia sasa umesajili maelfu ya Wakenya.

Katazo hilo lililotolewa na serikali litaendelea kutekelezwa hadi mashirika husika yatakapothibitisha kutokuwepo kwa hatari yoyote ya kiusalama .

“Vyombo husika vya usalama, huduma za kifedha na ulinzi wa data vimeanza uchunguzi ili kubaini ukweli na uhalali wa shughuli zilizotajwa, usalama na ulinzi wa takwimu zinazokusanywa , na jinsi wahusika wanavyokusudia kutumia data,” imesema taarifa hiyo.

“Zaidi ya hayo, itakuwa muhimu kwamba uthibitisho wa usalama wa umma na uadilifu wa miamala ya kifedha inayohusisha idadi kubwa ya raia utolewe kwa njia ya kuridhisha mapema.”

Kindiki aliongeza kuwa iwapo mtu yeyote atapatikana kusaidia au kujihusisha zaidi na shughuli hizo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya