ZINAZOVUMA:

Kenya yakanusha kudukuliwa na China

Kenya imekanusha kudukuliwa na China kwa miaka mitatu kama ambavyo...

Share na:

Kenya imekanusha madai ya kudukuliwa na Wachina baada ya Shirika la Habari la Reuters kuripoti kwamba mashambulizi hayo yalilenga idara za serikali ya Kenya kwa muda wa miaka mitatu.

Katika taarifa iliyotolewa Alhamisi jioni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Raymond Omollo, imesema madai yaliyowasilishwa kwenye kifungu hicho hayakuthibitishwa na watu husika kutoka kwa serikali ya Kenya na Uchina.

Ripoti hiyo ilidai kuwa udukuzi huo uliendelea kwa miaka mitatu ukilenga wizara nane za Kenya na idara za serikali ikiwa ni pamoja na ofisi ya rais na Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS).

Kisha ilihusisha mashambulizi hayo na madeni ya Kenya huku China ikidai kuwa ilitaka kupata taarifa kuhusu deni inayodai kwa Kenya kama kiungo cha kimkakati katika Mpango wa Rais Xi Jinping wa mtandao wa miundombinu wa kimataifa wa Belt and Road Initiative.

Hata hivyo kwa upande mwingine ubalozi wa China nchini Kenya ulipinga taarifa hiyo iliyotolewa na ‘Reuters’ na kusema haijawahi kufanya tukio kama hilo.

Endelea Kusoma

Anguko la mfumo wa Crowdstrike umesababisha kapuni nyingi duniani kushindwa kutoa huduma

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya