ZINAZOVUMA:

Kenya yafungua shule baada ya mafuriko makubwa

Share na:

Shule nyingi nchini Kenya zimefunguliwa tena leo Jumatatu ya Mei 13, baada ya kufungwa mara mbili kutokana na mafuriko yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 260.

Kenya na maeneo mengine ya Afrika Mashariki yalizidiwa na mafuriko, huku zaidi ya watu 150,000 waliokimbia makazi yao wakiishi katika kambi kote nchini Kenya.

Hata hivyo bado wazazi wanahofia usalama wa watoto wao, hasa katika miundombinu ya kujifunzia na mazingira vilivyoathiriwa na mafuriko.

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alisema kuwa, asilimia 95 ya shule ziko tayari kurejea kwa muhula wa pili, ila hali katika baadhi ya taasisi za elimu katika kaunti saba inachunguzwa ili kuhakikisha usalama wa watoto.

Taarifa hiyo ya waziri Machogu iliyoripotiwa na vyombo vya habari iliendelea kusema kuwa “uamuzi wa kufungua tena shule unafuatia ushauri wa Idara ya Hali ya Hewa ya Kenya, kwamba mvua kubwa iliyonyesha kwa muda mrefu imepungua”.

Chama cha Kitaifa cha Walimu wa Msingi nchini (KNUT), kimetaka serikali kutumia defha za mfuko wa elimu ili kukarabati shule zilizoathiriwa na mafuriko ila zifunguliwe haraka.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia aonekana kwenye hotuba yake kupitia mitandao wiki 3

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya