ZINAZOVUMA:

Kamati ya kudumu ya bunge ya utawala, katiba na sheria yakoshwa na ujenzi wa kituo jumuishi cha utoaji haki

Kamati ya kudumu ya Bunge ya utawala, Katiba na Sheria,...

Share na:

Kamati ya kudumu ya Bunge ya utawala, Katiba na Sheria, imesema Rais Samia Suluhu Hassan amesogeza nyezo na miundombinu ya utoaji haki kwa watanzania ili kurahisisha huduma kwa wananchi.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Utawala, Katiba na Sheria Joseph Mhagama wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa vituo vya haki jinai na kugawa vifaa vya tehama katika magereza ya wilaya ya Njombe na ludewa mkoani Njombe.

Amesema Mahakama za mwanzo zinajengwa lakini ujenzi wa kituo jumuishi cha utoaji haki ni moja kati ya ubunifu mkubwa ambao umetendeka na serikali ya awamu ya sita.

“Mmeona tangu Mahakama za mwanzo zinajengwa lakini kituo hiki jumuishi cha utoaji haki ni moja katika ubunifu mkubwa ambao umetendeka na serikali ya awamu ya sita hayo ni baadhi ya mambo machache ambayo mnaweza kuyashuhudia kwa macho yenu,”alisema Mhagama.

Amesema ujenzi wa kituo hicho ni hatua kubwa katika kuboresha mifumo ya utoaji haki nchini hivyo kuendelea kuijenga Tanzania ambayo ina hali ya utulivu na amani ya kutosha.

Alisema kamati hiyo inampongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa alioufanya ambao unakwenda kuboresha maisha ya watanzania.

“Kuhusu magereza wabunge tunaomba tuiagize serikali hapa kwamba baada ya kumaliza vikao vya bajeti kwa maana bunge la bajeti kuhitimishwa tungependa wizara kwa sababu tulishapanga huko mwanzo kwamba tutembelee mahaabusu na magereza,” alisema Mhagama.

Aliongeza”Iliratibiwa wakati fulani na DPP kutoka na kukosekana kwa muda lakini sasa mmekwenda kuwekeza huko na kuna changamoto mbalimbali ambazo tulitamani tuzijue ili tuweze kuishauri serikali,” alisema Mhagama.

Amesema awali waliangaika kutafuta bajeti ya DPP ili kuharakisha mashauri kwa sababu ya mrundikano wa mahabusu lakini ilibainika kuna changamoto za miundombinu ambazo hadhikizi mahitaji ya baadhi ya mahabusu aidha kwa kuzingatia jinsia zao au kwa kuzingatia jinsi.

Awali Waziri wa Katiba na Sheria balozi Dk.Pindi Chana alisema wizara hiyo imedhamiria kuhakikisha kuwa utawala wa sheria unakuwa miongoni mwa vipaumbele ili wawekezaji wakifika nchini wawe na imani kuwa nchi ina amani.

“Tunataka watanzania waishi kwa amani na uhuru kusiwepo na changamoto za jinai na pale zinapokuwepo tuwe na miundo mbinu za kudhibiti na kukabiliana nazo” alisema Chana.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka aliishukuru kamati hiyo kwa kutembelea miradi ndani ya mkoa wa Njombe kwani kufanya hivyo ni kwenda na falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha mradi inafuatiliwa.

“Natoa rai kwa wabunge kutumia nafasi hii kwa kutumia fursa ya kuja kuwekeza mkoani Njombe kwani kuna fursa nyingi za uchumi” alisema Kasongwa.

Endelea Kusoma

Mwanzilishi wa Telegram mwenye asili ya kirusi amekamatwa nchini Ufaransa siku ya

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya