ZINAZOVUMA:

Imamu achomwa kisu akiswalisha.

Imamu nchini marekani ameshambuliwa na kuchomwa kisu mgongoni wakati akiswalisha...

Share na:

Jumapili ya tarehe 9 Aprili 2023 Imam Sayeed Elnakib (65) wa msikiti wa Omar nchini marekani alishambuliwa na kuchomwa kisu wakati akiswalisha swala ya Al fajri.

Imamu huyo kwa sasa yupo katika kituo cha matibabu na hali yake inaendelea kuimarika huku kijana aliyehusika na tukio hilo akiwa katika mikono ya polisi.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 32 alijaribu kukimbia baada ya tukio hilo lakini waumini walifanikiwa kumdhibiti na kumfikisha katika vyombo vya usalama.

Waumini wa msikiti huo wanasema kuwa kijana huyo si muumini wa hapo na hakuwahi kuonekana kabla ya tukio hilo.

Endelea Kusoma

Waziri Mkuu wa Slovakia amejeruhiwa vibaya katika jaribio lakutaka kumuua kwenye mji

Chaguo la Mhariri

Habari Mpya