Muhubiri maarufu duniani wa dini ya Kiislam na Imaam wa Msikiti wa Al-Tawheed uliopo New Jersey, nchini Marekani Sheikh Abdullah Kamel amefariki dunia jana Alhamisi, Aprili 27, 2023
Kifo cha Sheikh Abdullah Kamel kimetangazwa leo, Alhamisi asubuhi tarehe 27 ya Aprili 2023 huko Marekani katika ukurasa rasmi wa msikiti aliokuwa anaouongoza ambao uliandika “sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea”.
Hata hivyo hakuna yeyote aliyeeleza sababu ya kifo cha Sheikh Abdullah Kamel huko Amerika, si kutoka kwa vyanzo rasmi au vya familia.
Sheikh Abdullah Kamel atakumbukwa kutokana na umahiri wake katika fani ya usomaji wa Quran tukufu na anachukuliwa kuwa imamu stadi na anayeheshimika sana nchini Marekani.